1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho kwa watoto Somalia

20 Julai 2011

Watoto nchini Somalia hawamo tu katika hatari ya baa la njaa, bali pia kusajiliwa na wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu

https://p.dw.com/p/11zxb
Watoto wengi Somalia wanakosa haki zao kwa kitisho kinachowakumbaPicha: picture-alliance / dpa

Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, imeyasema hayo mapema hii leo.

Somalische Flüchtlinge in Kenia
Picha: AP

Kundi hilo lililo na makao yake mjini London Uingereza, limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulinda haki za watoto katika nchi hiyo iliogawanyika kivita, ambapo maelfu ya watu wanakimbia ukame mkubwa.

Umoja wa mataifa hapo jana ulitangaza kuwa kiasi ya wasomali 4000 wanakimbia nchi hiyo kila siku wakati Ukame na baa la njaa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 7 kila siku kutoka kila wakaazi 10,000.

Huku idadi kubwa ya vifo, ikiwa ni ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 5.

Mwandishi: Maryam Abdalla/dpa, afp, reuters
Mhariri:Hamidou,Oummilkheir