1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kituo cha Matangazo cha RFI yasitishwa nchini DRC

6 Januari 2012

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewasilisha malalamiko yake kwenye halmashauri ya upashaji habari kwa kupinga kile serikali imekiita ni ujumbe wa ubaguzi na wa chuki za kikabila unaotolewa na redio ya RFI.

https://p.dw.com/p/13fDe
Logo RFI
RFI (Radio France International) imesitishwa nchini DRC

Toka wiki iliyopita serikali ya Kongo ilisitisha matangazo ya RFI kwa masafa ya FM kote nchini. Mashirika ya haki za binadamau yamelalamikia hatua hiyo ambayo yameieleza kuwa ni kuwanyima wananchi wa Kongo haki ya kupata habari.

Taarifa kamili na mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Othman Miraji