1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utalii wa kimazingira Kaskazini mwa Ujerumani

17 Novemba 2015

Utalii wa kimazingira ni njia mojawapo ya kuwahamasisha watu kuyalinda mazingira hayo wakielewa umuhimu wake. Ni katika mukhtadha huo, kwamba utalii wa aina hiyo umeshamiri katika maeneo ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1H7RK
Seehundstation in Norddeich
Watalii wakiwatazama sili mayatima kupitia ukuta wa kiooPicha: DW/D. Gakuba

Kwa wajerumani, utalii katika miradi ya mazingira imekuwa kama tabia kwa wengi, na tabia hiyo husaidia kuweka uelewa na hamasa ya kila mmoja kuyalinda mazingira na viumbe asilia wanaoishi katika mazingira hayo.

Sehemu moja yenye vivutio vingi vya kimazingira ni mji wa Norddeich, ambao idhaa yako ya Kiswahili iliutembelea hivi karibuni. Tafadhali sikiliza makala hii ya Sura ya Ujerumani iliyoandaliwa kutokana na ziara hiyo.

Seehundstation in Norddeich
Nje ya kituo hicho maalum cha kuwatunza sili mayatimaPicha: DW/D. Gakuba

Inahusu matunzo ya ufukwe wa tope katika Bahari ya Kaskazini, na Kituo cha kuwatunza mayatima wa wanyama wa majini waitwao sili, au seals kwa lugha ya kiingereza. Makala hiyo imeandaliwa nami Daniel Gakuba.