1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kituo kipya cha matangazo chafunguliwa Sierra Leone

Oumilkher Hamidou15 Juni 2010

Sierra Leone yaahidi kituo huru cha matangazo kwa lugha ya kiengereza kitakua cha wananchi wote kwa lengo la kueneza utawala bora na uhuru wa mtu kutoa maoni yake

https://p.dw.com/p/NrYc
Msikilizaji wa kituo kipya cha matangazo cha Sierra LeonePicha: AP

Sura ya vyombo vya habari nchini Sierra Leone imezidi kutakata baada ya kufunguliwa kituo cha kwanza cha matangazo ya umma. Kituo hicho kipya cha matangazo ya radio kimefunguliwa rasmi jana na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon. Hayo ni matokeo ya muungano kati ya kituo cha matangazo ya radio kinacho simamiwa na Umoja wa mataifa na kile kinachosimamiwa na serikali ya Sierra Leone. Kituo hicho cha matangazo-"Sierra Leone Broadcasting Corporation" kimeidhinishwa na bunge April mwaka huu. Kinatarajiwa kutoa habari zisizoelemea upande wowote na kuburudisha wananchi kote nchini Sierra Leone.

Mojawapo ya idhaa zinazotangaza kwa lugha ya kiengereza katika eneo la Afrika Magharibi-Kituo cha matangazo ya Radio cha Sierra Leone (SLBS) kimeanzishwa mwaka 1934 katika koloni hilo la zamani la Uengereza. Tangu kilipofunguliwa, kituo hicho kimekua kikidhibitiwa na serikali na kutumiwa kwa sehemu kubwa kueneza sera za serikali na mafanikio yake. Hadja Kadie Johnson, mkuu wa masuala ya akinamama katika kituo cha matangazo cha-Sierra Leone Broadcasting Service, SLBS, anachambua jinsi hali namna ilivyokua serikali ilipokua ikidhibiti taasisi hiyo na jinsi anavyojisikia hii leo,miaka 24 baadae:

"Kwakua kitakua huru hatutokua na wasi wa kusema chochote tunachotaka kusema, kama hatutaitusi serikali. Tulipokua katika enzi za SLBS, tulibidi kutahadhari na kuepukana na jambo lolote linaloweza kuiudhi serikali."

Wizara ya habari na mawasiliano ilipewa jukumu la kusimamia shughuli za utawala na kuchunguza yaliyomo katika vipindi vya kituo cha zamani cha SLBS. Kwa hivyo, rais wengi wa Sierra Leone wanasema haitakua rahisi kwa serikali ya sasa kuendeleza ukaguzi wake. Alhaji Ibrahim Ben Kargbo, ambae ni waziri wa habari na mawasiliano, amehakaikisha kwamba serikali inawajibika katika kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na haitoingilia kati katika shughuli za kituo hiki kipya.

"Serikali haitojihusisha hata kidogo na mambo ya utangazaji-tutawaachia viongozi wafanye shughuli zao ipasavyo na watakua na uhuru. Bora niseme pia kwamba safari hii tunataka kuhakikisha kwamba kituo cha taifa cha matangazo kinachomilikiwa na umma kitakua cha uwazi zaidi kwa namna ambayo serikali, upande wa upinzani, mashirika ya huduma za jamii, kila mmoja atakua na uhuru wa kukitumia ili kueneza utawala bora na uhuru wa mtu kutoa maoni yake."

Hata utaratibu wa kuwachagua wafanyakazi utakua huru.Wafanyakazi wote wa kituo cha zamani cha SLBS wamejiuzulu.

Mwandishi: Sarah Bomkapre Kamara/Hamidou Oummilkheir

Mpitiaji: Miraji Othman