1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klitschko kutetea taji la IBF dhidi ya Kubrat Pulev

9 Mei 2014

Bingwa wa ndondi wa ulimwengu katika uzani wa juu Vladmir Klitschko ameamrishwa kulitetea taji lake la Shirikisho la Kimataifa la Ndondi – IBF dhidi ya Kubrat Pulev wa Bulgaria ambaye hajawahi kushindwa pigano lolote.

https://p.dw.com/p/1BxFH
Klitschko bleibt Weltmeister - Leapai chancenlos
Picha: Reuters

Klitschko aliyatetea mataji yake ya WBA na WBO pamoja na mkanda wa IBF wiki mbili zilizopita alipomwangusha sakafuni katika raundi ya tano bondia Alex Leapai wa Australia.

Hilo lilikuwa pigano la lazima la kutetea taji lake la WBO, na sasa Shirikisho la IBF limetangaza Pulev mwenye umri wa miaka 33 kama mpinzano wao wa lazima.

Pulev ameukaribisha uamuzi huo akisema kwamba hiyo ni zawadi yake kubwa ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Pulev anasema alishuhudia pigano la Klitschko na Leapai na ni kweli kwamba Klitshcko hakuwa na kibarua chochote dhidi ya mpinzani huyo.

Lakini anasema pigano lake na Mu Ukraine huyo litatimiza ndoto yake na kuuonyesha ulimwengu kuwa Klitschko siyo mashine isiyoweza kushindwa. Promota wa Pulev amesema tayari mazungumzo yameanza kuhusu pigano hilo dhidi ya Klitschko.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu