1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Klabu bingwa Afrika

1 Agosti 2008

Al Ahly ina miadi na Asec Abidjan katika kombe la Afrika wakati Rais wa china hataki siasa katika olimpik.

https://p.dw.com/p/EoVz
Rais Hu JintaoPicha: AP

Kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani Afrika charudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii kwa miadi kati ya Al Ahly ya Misri na ASEC Abidjan ya Ivory Coast lakini bila stadi Aboutraika.

Tanzania imetangaza kikosi chake cha wanariadha 10- wakiwemo waogoleaji 2 kwa michezo ya Olimpik ya Beijing.

Rais wa China Hu jintao ametoa mwito wa kutenganishwa siasa na Olimpik,jee hii yawezekana ? Halima Nyanza atawaarifu.

Ni Ramadhan ali nikiwakaribisha katika ulimwengu wa michezo wiki hii tukituwama zaidi leo katika michezo ijayo ya Olimpik ya Beijing:

Tangu mwenge wa olimpik kupita katika miji ya magharibi ukiwa njiani kuelekea Beijing,kwa ufunguzi wa michezo ya 29 ya olimpik ijumaa ijayo ,siasa zimekuwa zikiandamana na michezo ya Beijing , 2008.China imetuhumiwa kuvunja ahadi ilizotoa ilipotunukiwa nafasi ya kuiandaa michezo hii. Ikiweka vikwazo vya habari katika mtandao wa Internet ambavyo sasa imeviondoa. Ikaahidi pia kukuza haki za binadamu.

Ijumaa ijayo,marais na viongozi wa serikali kiasi cha 80 pamoja nao George Bush wa Marekani, watahudhuria ufunguzi rasmi katika uwanja mkuu wa kisasa kabisa wa Beijing.Machafuko ya Tibet yaliozimwa kwa mkono wa chuma na vikosi vya usalama vya China na ukaguzi uliofuatia wa habari kutoka Beijing kupitiab mtandao wa Internet, kumeengeza kama inavyotokea mara kwa mara, mchezo 1 zaidi katika kalenda ya olimpik 2008-mchezo wa siasana Olimpik.

Rais wa China Hu Jintao, alitoa mwito ijumaa kuweka kando siasa na olimpik.

Je, itawezekana ? Mara nyingi michezo ya olimpik imekuwa ikiandamwa na siasa: Ilikua hivyo, Mexico City, 1968, Munich 1972 na Montreal ,1976 ilipotishiwa kugomewa na wanariadha wa Afrika.Na halkadhalika, tulijionea Marekani na washirika wake wakiigomea michezo ya Moscow, 1980 baada ya Urusi kuivamia Afghanistan. Urusi na washirika wake nao wakaisusia michezo ya 1984 ya Los Angeles.

Haikusangaza kwahivyo, kumsikia jana Rais wa China Hu Jintao, kutoa mwito kutenga siasa nje ya Olimpik.Akijribu hapo kuzima ila kali zilizotolewa

ulimwenguni wiki kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ilioianika hadharani vipi china inavyoendesha mambo ndani na nje.

Baadhi ya mawasiliano ya Internet yalizimwa ,lakini kufuatia malalamiko makali yalirejeshwa hapo ijumaa .Hatahivyo, rais wa China Hu jintao, alionya kwamba ni kinyume na moyo wa olimpik kuchanganyisha siasa na michezo na kulketa maswali kama hayo ya kisiasa usoni mwa mji wa Beijing hakusaidii kitu.

Michezo ya Beijing inatumainiwa na wenyeji China, kuonesha nguvu zake zinazoongezeka ulimwenguni kama dola kuu. Kiasi cha waandishi habari 20,000 wa Radio,TV na magazeti wamo kuwasili Beijing na uongozi wa chama kikuu cha kikominist cha China unajikuta unachunguzwa barabara kuliko wakati wowote kabla tena kutoka ndani ,kwani imewafungulia mlango waandishi hao.China imejaribu sana kuwalazimisha kushughulikia spoti tu na sio siasa na haki za binadamu, bila ya mafanikio.

Kuanzia mkomoto huko Tibet hadi malalamiko yalioandamana na mwenge wa olimpik,usuhuba wake na Sudan, inayolaumiwa kukanyaga haki za binadamu mkoani Dafur, siasa imekua ikitokeza kichwa chake mara kwa mara katika michezo hii.

Hatua ya China kuzima mawasiliano ya mtandao wa Internet yaliifedhehesha mno Halmashauri Kuu ya Olimpik Ulimwenguni (IOC).

Rais wa IOC Jacques Rogge mwezi uliopita aliahidi kwamba vyombo vya habari vya kigeni vingepewa uhuru kamili katika Internet.

Kufuatia malalamiko, jana mtandao wa shirika linalotetea haki za binadamu ulimwenguni-Amnesty International, shirika la maripota wasio na mipaka na hata kituo hiki Deutsche Welle yameondolewa vizuwizi hivyo.

Njia sasa yaonesha iko wazi kwa ufunguzi ijumaa ijayo,lakini tusitumai tu kuwa risasi za mwisho katika vita kati ya siasa na Olimpik zimefyatuliwa.

Hii inatukumbusha onyo kali la rais wa zamani wa IOC-Halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni, marehemu Avery Brundage: yeye alisema:

"Zamani huko Olympia wakati wa Olimpik, ugomvi wote ukiwekwa kando ili kushiriki katika Olimpik, leo watu wanaweka kando olimpik kwenda vitani."

Tubakie katika medani ya Olimpik:

Kikosi cha wanariadha 10 wa Tanzania kikiingiza waogoleaji 2 kitaondoka jumatatu hii kuelekea Beijing kwa michezo ya olimpik.Ni kitambo kirefu tangu katibu wake wa sasa wa Kamati ya olimpik, Philbert Bayi, bingwa wa zamani wa rekodi ya mita 1.500 alipoipatia medali ya fedha Tanzania katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi mjini Moscow.Mwenzake Suleiman Nyambui akaambulia nae pia medali ya fedha katika mbio za mita 5000.

Tanzania ina kiu bado cha medali ya dhahabu ya olimpik na je, vipi mwaka huu itatamba katika medani ya riadha na vipi baadhi yamabondia wake waliotiwa nguvuni huko Mauritius kwa tuhuma za madaw aya kulevya:

Dimba:Kombe la Afrika la klabu bingwa; Wakati kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika mashariki na kati kilimalizika kwa ushindi wa tusker ya kenya dhidi ya Ugandan Revenue Authority, jumapili iliopita, kil cha kombe la klabu bingwa kinaendelea:

Al Ahly ya Misri ilicheza duru iliopita na mahasimu wao wa nyumbani Zamalek.Leo wana miadi na ASEC Abidjan ya Ivory Coast lakini bila ya jogoo wao Mohammed Aboutraika na Emad Motaeb.mchezaji wa kiungo Aboutraika bado hakupona sawa sawa goti lake lililohitaji matibabu hapa Ujerumani wakati mshambulizi Moteab pia anaugua .Kwahivyo, leo hakuna materemko kwa Al Ahly mjini Abidjan.

Taarifa nzuri kwa mabingwa hawa mara 5 wa Afrika-al Ahly ni kuwa stadi wao wa kiungo kutoka Angola, Gilberto sasa ni fit kucheza tena .Gilbert aliukosa ule mpambano wa kwanza na Zamalek ulioleta ushindi kwa Al Ahly wa mabao 2-1 mwishoni mwa wiki iliopita.

Al Ahly iliwasili Abidjan tangu alhamisi.Aboutraika ndie alietia bao la ushindi dakika 5 kabla kipindi cha mapumziko dhidi ya ASEC katika hatua sawa na hii ya kinyan'hganyiro cha kombe hili.Al Ahly ikaibuka mwishoe,makamo-bingwa.

Zamalek iliotawazwa mabingwa wa afrika mara 5 kama Al Ahly, wana miadi kesho jumapili na Dynamo ya zimbabwe na kila moja imejitapa hadharani kuwa itatamba.Klabu ya harare-Dynamo ilizuisha msangao mwaka huu ilipofunga safari hadi Tunisa miezi 2 iliopita na kuizaba huko klabu bingwa etoile du Sahel bao 1:0.

TP Mazembe ya jamhuri ya kidemokrasi ya kongo na Enyimba ya Nigeria ambazo pamoja na Al Ahly ndizo pekee zilizoshinda kombe hili mara 2 mfululizo zinacheza nyumbani.

Enyimba inaangaliwa ni kitisho kikubwa kwa Al Ahly ina miadi nyumbani na Contonsport Garoua ya Kamerun kesho mjini Aba wakati Mazembe wamewakaribishja Al hilal ya Sudan mjini Lumbubashi jioni hii.