1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la mashirikisho

19 Juni 2009

Bafana bafana wapambana leo na Spain.Iran na NZ.

https://p.dw.com/p/IUn1
Fernando Torres atatamba tena leo ?Picha: AP

Kesho- "asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu, atie gongo- mkutano uwanjani mjini Pretoria. Mabingwa wa dunia Itali, wanapambana na mabingwa wa Kombe la mashirikisho- Brazil katika changamoto ya kufa-kupona kwa Itali .Leo (Jumamosi) ni zamu ya ya mabingwa wa Asia-Iraq wenye miadi na New Zealand leo usiku huku mabingwa wa Ulaya Spian wakiumana na wenyeji Bafana bafana. Finali ya kombe hili ni Juni 28.

Mwishoni mwa wiki hii, sambamba na Kombe la mashirikisho, kinaendelea kinyanganyiro cha kufuzu kwa Kombe la Dunia na la Afrika kanda ya Afrika: Simba wa nyika -Kamerun wana miadi na Gabon wakati Tembo wa Ivory Coast leo wanaitembelea Burkina Faso.

Mabingwa wa Afrika Misri, waliowasangaza mashabiki wa kombe hili kwa kuwatoa jasho mabingwa Brazil na mabingwa wa dunia Itali,wana miadi kesho na Marekani uwanjani mjini Rustenburg kuania nafasi yao ya nusu-finali.

Mafiraouni,waliwasili Afrika kusini baada ya kuzabwa mabao 3-1 na Algeria katika kinyanganyiro cha kuania tiketi za Kombe lijalo la dunia.Lakini, mara tu kuteremka uwanjani huko Afrika Kusini,kikosi hiki cha kocha Hassan Shehata,kiliwafunga vinywa wakosoaji na kutamba mbele ya Brazil hadi dakika ya 90 ya mchezo walipolazwa kwa bao la kutatanisha la mkwaju wa penalty.

Bao la kipindi cha kwanza alilotia Mohamed Homos dhdi ya mabingwa wa dunia itali mjini Johannesberg juzi ,limezusha hali ya kutatanisha katika kundi hili B huku timu 3 isipokuwa Brazil, kila moja yaweza kucheza nusu-finali baada ya mapambano 2 ya kesho.

Ushindi wa Misri dhidi ya Marekani utawapa wamisri pointi 6 na tiketi ya nusu-finali ikiwa Itali ikilazwa na mabingwa Brazil. Ushindi wa wataliana lakini, utaziweka timu zote 3 sawa na hivyo tofauti ya magoli itaamua nani anasonga mbele katika kundi hili.

Katika mpambano wapili-Brazil na Itali, Itali lazima ishinde la si hivyo, itaaga mashindano.

Usiku wa leo (Jumamosi) katika kundi A,mabingwa wa Asia-"simba wa Mesopotemia"-Irak wanacheza na "All Whites"-New Zealand.Sambamba na mpambano huo wa saa tatu-unusu usiku,wenyeji Bafana Bafana-Afrika kusini, wanachuana na mabingwa wa Ulaya Spain.Spian wameshakata tiketi yao ya nusu-finali,Bafana Bafana wataridhika tu wakitoka suluhu kwani tayari wana pointi 4.

Katika kinyanganyiro cha kanda ya Afrika cha kuania kufuzu kwa Kombe lijalo la dunia 2010, ukweli leo utadhihirika kwa timu iliozusha msangao ya Burkina Faso inayoingia uwnajani jioni hii na Tembo wa Corte dźiviore.Timu zote mbili zimezishinda guinea na Malawi na mapambano yao 2 hapo septemba-moja mjini Abidjan na Ouagadougou yataamua nani anakwenda Afrika Kusini kwa Kombe la kjwanza barani Afrika.

Kocha wa Super eagles-Nigeria, Shaibu Amodu amevuta pumzi pale timu yake ilipomudu sare ya 0:0 na Msumbiji na baadae kuilaza Harambee Stars-Kenya mabao 3-0 mjini Abuja.

Zambia inaonana na Algeria,iliowalaza mabingwa wa Afrika Misri 3:1 duru iliopita.Morocco iliotoka sare na Simba wa nyika-Kamerun ina miadi nyumbani na Togo wakati Harambee Stars wanacheza na Msumbiji mjini Nairobi.Sudan inaahidi kutamba mjini Oumduraman mbele ya Ghana.Mali na Benin zinacheza Bamako.Wakati Malawi iko Conackry kutimiza miadi na Guinea.

Mwandishi: Ramadhani Ali /RTRE

Mhariri: Josephat Charo