1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Ulaya:Ujerumani yacharuka ugenini

13 Oktoba 2010

Ujerumani imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za kombe a mataifa ya Ulaya baada ya kuichabanga Kazakhstan mabao 3-0.

https://p.dw.com/p/Pd9A
Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Mueller (kulia) akifyatua kombora kuelekea katika mlango wa KazakhstanPicha: picture alliance/dpa

Kwa ushindi huo Ujerumani sasa inaongoza kutoka katika kundi lake la A ikiwa na pointi 12, ikifuatiwa na Austria yenye pointi 7.Yalikuwa ni mabao ya Miroslav Klose, Mario Gomez na Lukas Podoski yaliyopachikwa katika kipindi cha pili ambayo yaliweka kileleni Ujerumani.

Serbien Hooligans EM Qualifikation Fußball Ausschreitungen FLash-Galerie
Washabiki wa Serbia wakipambana na polisi wa Italia, kabla ya kuanza kwa pambano lao katika uwanja wa Luigi Ferraris huko Genoa, Italia ,Picha: AP

Katika mechi nyingine, Washabiki wa Serbia walisababisha mpambano kati ya timu yao na Italia kuvunjwa dakika sita tu tokea kipyenga cha kuanzisha mpambano kupulizwa kutokana na kufanya vurugu.Washabiki hao wa waserbia walirusha fataki uwanjani halikadhalika kwa washabiki wa Italia.Serbia sasa inakabiliwa na kitisho cha kufungiwa.

Ama Uingereza ikicheza nyumbani ilishindwa kutamba baada ya kubanwa na Montonegro na kulazimishwa kutoka suluhu bin suluhu, huku Ufaransa ikiichapa Luxembourg mabao 2-0.

Uholanzi ikicheza nyumbani ilitamba kwa kuishindilia Sweden bila huruma mabao 4-1, ushindi kama huo pia ikiupata Uswisi nyumbani dhidi ya Wales.

Mabingwa wa dunia Huspania iliwalazimu kufanya kazi ya ziada kuweza kuifunga Scotland nyumbani kwao mabao 3-2.Nayo Ureno ikihitaji mabao ya Christiano Ronaldo , Raul Meireles , Helder Postiga.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters/DPA

Mhariri:Mohamed Abdulrahman