1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano juu ya uwekezaji Afrika Mashariki

29 Julai 2009

Kongamano la Pili la Kiuchumi lililoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki limeanza leo mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/Izjs
Jiji la Nairobi kunakofanyika kongamano la uwekezajiPicha: DW
Kongamano hilo la siku tatu lililofunguliwa na Marais wa Jumuiya hiyo linahudhuriwa na zaidi ya wajumbe elfu moja wakiwemo wawekezaji na wanabiashara kutoka Afrika, Ulaya na Marekani. Mkutano huo ambao ni wa pili kufanyika tangu jumuiya hiyo ifufuliwe ni kuwahamasisha wawekezaji juu ya nafasi zilizopo za uwekezaji katika eneo zima la Afrika Mashariki na kutafuta mbinu za kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa kote Duniani. Mwandishi wetu kutoka Nairobi Alfred Kiti ametuandalia taarifa ifuatayo. Mtayarishaji:Alfred Kiti Mpitiaji:Othman Miraji