1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo Kinshasa yaajipatia waziri mkuu mpya

Hamidou, Oumilkher11 Oktoba 2008

Adolphe Muzito ateuliwa kushika wadhifa ulioachwa na Antoine Gizenga

https://p.dw.com/p/FY3t

Kinshasa:


Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo amemteuwa Adolphe Muzito awe waziri mkuu,baada ya Antoine Gizenga kujiuzulu September 25 iliyopita.

Adolphe Muzito,mwenye umri wa miaka 51,aliyekua waziri wa bajeti katika serikali ya waziri mkuu aliyejiuzulu Gizenga,ni mfuasi wa chama cha "Wanalumumba walioungana-Parti Lumumbiste Unifié-(PALU),kama alivyokua mtangulizi wake.

Mnamo mwaka 2006,chama cha PALU kilitiliana saini makubaliano pamoja na rais Joseph Kabila,cheo cha waziri mkuu wakabidhiwe wao ili badala yake wamuunge mkono rais Kabila katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Waziri mkuu mteule Muzito anakabiliwa jukumu kubwa;mapigano kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi yamepamba moto tangu Agosti iliyopita huku aswili mia 75 ya wakaazi milioni 60 wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wanasemekana wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.