1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini kurusha satelaiti 3 mwaka 2024

Lilian Mtono
31 Desemba 2023

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema taifa hilo linajiandaa kurusha satelaiti tatu za kiintelijensia kwa mwaka 2024,

https://p.dw.com/p/4ajrn
Pyongyang, Korea Kaskazini 2023 | Kim Jong-un atoa wito wa maandalizi ya vita
Kim Jong-un akihudhuria kikao cha siku ya pili cha mkutano wa mwisho wa mwaka wa Kamati Kuu ya Chama tawala nchini humo, mjini Pyongyang mnamo Desemba 27, 2023. Picha hii ni kwa hisani ya kituo rasmi cha Televisheni cha Korea Kaskazini.Picha: Yonhap/picture alliance

Uamuzi wa kurushwa kwa satelaiti hizo za ujasusi ulitangazwa katika mkutano wa chama tawala na kuwa moja ya uamuzi muhimu wa kisera kwa mwaka 2024, limesema shirika la habari la serikali, KNCA.

Mkutano huo wa siku tano ulihudhuriwa pia na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.

Kim aidha, alitangaza mipango ya kutengeza ndege zisizo na rubani, kuendeleza uwezo wa vita vya kielektroniki, pamoja na kuimarisha nguvu za nyuklia na makombora.

Mwaka 2023, Taifa hilo lilivunja rekodi ya majaribio ya silaha na inalenga kuongeza uwezo wake wa kijeshi, huku Japan, Korea Kusini na Washington wakiimarisha ushirikiano unaolenga kuikabili mikakati hiyo ya Pyongyang.