1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini kupeleka jeshi mpakani mwa Korea Kusini.

Saumu Mwasimba
23 Novemba 2023

Korea Kaskazini imesema itapeleka jeshi pamoja na silaha mpya katika mpaka wake na jirani yake Korea Kusini,siku moja baada ya serikali ya mjini Seoul kufuta sehemu ya makubaliano ya kijeshi yaliyofikiwa mwaka 2018.

https://p.dw.com/p/4ZLcu

Korea Kusini ilitangaza uamuzi wake wa kusitisha makubaliano hayo kupinga hatua ya Pyongyang ya kurusha satelaiti yake ya ujasusi. Wizara ya ulinzi ya Korea Kaskazini kupitia taarifa yake iliyochapishwa na shirika la habari la KCNA imesema nchi hiyo itarudisha harakati zote za kijeshi ilizokuwa imezisimamisha chini ya makubaliano na jirani yake Korea Kusini, ambayo yalidhamiriwa kuumaliza mvutano baina ya nchi hizo mbili katika eneo la mpaka wa pamoja.Korea Kaskazini ilirusha satelaiti ya Ujasusi Jumanne, ikiwa ni jabirio lake la tatu ndani ya mwaka huu baada ya kushindwa mara mbili.