1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yaionya Marekani

Lilian Mtono
27 Aprili 2024

Korea Kaskazini imeishutumu Marekani hii leo kwa kuingiza siasa kwenye masuala ya haki za binadamu nchini humo na kulaani kile ilichokiita siasa za uchochezi na njama.

https://p.dw.com/p/4fFC6
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un
Korea Kaskazini imeionya Marekani juu ya kutumia siasa katika masuala ya haki za binaadamu na kuahidi kujilinda kikamilifuPicha: Uncredited/KCNA/KNS/dpa/picture alliance

Shirika la habari la serikali limemnukuu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini aliyemesema Pyongyang itafanya maamuzi magumu na thabiti ya kulinda uhuru wake na usalama katika kukabiliana na Washington inayotumia haki za binadamu kama chombo cha uvamizi dhidi ya Korea Kaskazini.

Msemaji huyo alisema hayo akiiangazia ziara ya mjumbe maalum wa haki za binadamu wa serikali ya Rais Joe Biden, Julie Turner, nchini Korea Kusini mwezi Februari na kujadili Korea Kaskazini.

Ripoti ya mwaka ya Wizara ya Mambo ya Nje imeonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu nchini Korea Kaskazini ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela, mateso na adhabu kali zinazotolewa na mamlaka.