1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kosovo isiharakishe kujitangazia uhuru

19 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJKy

Mawaziri wa Nje wa Umoja wa Ulaya wametoa mwito kwa atakaekuwa waziri mkuu mpya wa Kosovo kutoharakisha kujitangazia uhuru kutoka Serbia. Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,majadiliano ya kimataifa bado yanahitaji kupewa nafasi.Chama cha kiongozi wa zamani wa waasi wa Kosovo,Hashim Thaci kilishinda uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya Jumapili.

Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani Frankfurter Allgemeine Zeitung Thaci amesema, hataraji kuwa maafikiano yatapatikana kati ya Kosovo na Serbia.Yeye anagombea uhuru wa Kosovo kutoka Serbia lakini amesema,ataheshimu ajenda yo yote itakayopangwa na pande tatu zinazohusika na suala la Kosovo yaani Urusi,Umoja wa Ulaya na Marekani.