1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KPA wabebwa ubingwa wa FIBA Rwanda

6 Novemba 2023

Timu ya mpira wa kikapu Kenya Ports Authority (KPA) wanawake, watawazwa mabingwa wa Ukanda wa V wa Afrika katika shindano la mpira wa kikapu maarufu "FIBA African Women Basketball League,''

https://p.dw.com/p/4YSio
Visit Rwanda Sponsoring beim FC Arsenal
Picha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Imewabwaga Rwanda Energy Group (REG) timu ya nishati ya Rwanda kwa vikapu  87-53  jumamosi mjini Kigali.

Timu ya mpira wa kikapu Kenya Ports Authority  KPA imemaliza mechi zote bila kufungwa, katika mchezo wa fainali imeifunga Club ya nishati Energy  Group, kwa vikapu  87-53  jumamosi.

Soma pia: Rayon Sport yashindwa kutamba katika ligi kuu Rwanda

Timu ya Kenya Ports Authority  wanawake, imetawazwa mabingwa wa Ukanda wa V katika shindano la mpira wa kikapu maarufu'' FIBA Africa Women Basketball League'' kufuatia  ushindi wa vikapu  87-53 dhidi ya REG  Rwanda Energy Group Timu ya nishati ya Rwanda.

Kocha wa KPA Antony Ojukwu Oloo alisema ‘'Naweza kusema kuwa shindano lilikuwa gumu na limekuwa zuri ka sababu tulikuwa tumejitayarisha vya kutosha, nashukuru  pia  na ninapongeza wachezaji wangu na uongozi kwa jumla. Niseme pia kwamba ulinzi (defense yangu) imenisaidia sana kupata ushindi''

Kocha wa REG  mshindi wa pili Mukaneza Esperance, "Katika mchezo wa fainali tulianza na nguvu nyingi pamoja na kwamba kulikuwepo tofauti, imeonekana wapinzani walikuwa juu yetu, tulipambana hadi dakika ya mwisho. Tulikuwa na mchezaji  wetu hatari kwa jina Nyota Mireille ambaye hakucheza alipata jeraha." 

Timu hizo mbili  moja kwa moja zimefuzu kushiriki fainali ya kombe la Afrika  FIBA Africa Women Basketball League'  itakayofanyika nchini Misri tarehe 8-17, 2023.

Equit Bank ya Kenya wamemaliza kwenye nafasi ya tatu kufuatia ushindi wao dhidi ya timu ya Uganda ya JK Lady.

Mshindano hayo yaliyokuwa  yakifanyika Kigali kuanzia tarehe 28 Octoba  hadi 04 Novemba 2023 yametamatika mwishoni mwa juma.

Tuangazie upande wa soka, Torsten Frank Spittler mjerumani  mwenye umri wa miaka 61 ametangazwa  na Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA kuwa kocha mpya wa  Timu ya taifa ya soka ya Rwanda  Amavubi akichukua mikoba ya mhispania Carlos Alos Ferrer.

Spittler hana historia nzito ya ukufunzi. Hapo kabla alikuwa mkurugenzi wa ufundi  katika shirikisho la  soka nchini Msumbiji na Siera Leonne.

Aliwahi pia kuwa  mkufunzi  msaidizi wa timu ya taifa ya  Ujerumani kwa wachezaji walio chini ya miaka 16.

Rwanda ina kabarua kuchuana na Zimbabwe tarehe 15 Novemba 2023  kabla ya kuipokea Afrika ya kusini tarehe 21  mwezi huu mjini Huye kusini mwa Rwanda kusaka tikiti ya kombe la dunia mwaka 2026.

Mpira wa kikapu

 

//Christopher Karenzi (DW Kigali)