1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUALA LUMPUR: Malaysia yakumbwa na mafuriko.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaj

Malaysia imekumbwa na wimbi la pili la mafuriko na hivyo kuzidisha wasiwasi wa raia kuambukizwa maradhi.

Maafisa wamesema watu wawili wamefariki kutoka na homa inayosababishwa na maji machafu.

Watu zaidi ya elfu tisini walilazimika kukimbia makazi yao katika jimbo la Johor karibu na Singapore.

Mafuriko hayo yamelikumba eneo hilo punde baada ya watu kurejea katika makazi yao waliyokuwa wameyakimbia mwezi Disemba kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mito ifurike na watu kiasi kumi na saba wakafariki.