1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuala Lumpur.Mahadhir Mohamad alazwa hospitali.

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuf

Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohamad, amelazwa katika hospitali mji mkuu wa nchi hiyo Kuala Lumpur, baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Mmoja kati ya watoto wake amesema, baba yake mwenye umri wa miaka 81, yupo katika hali nzuri lakini atalazimika kubakia hospitali kwa siku chache.

Mahathir Mohamad ndie waziri mkuu aliushikilia wadhifa wa uwaziri mkuu kwa muda wa miaka 22, kabla ya kuachia madaraka mwaka 2003, na ni waziri pekee hadi hivi sasa nchini humo kushikilia wadhifa huo kwa muda mrefu.