1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Historia ya Google

Sekione Kitojo5 Novemba 2009

Google inashughulikia zaidi ya maulizo milioni 200 kwa siku.

https://p.dw.com/p/KPUp

Googe inashughulikia zaidi ya maulizo milioni 200 kwa siku, ama kwa wastani wa theluthi mbili ya utafutaji wa habari katika mtandao wa internet kwa jumla.

Kuanzia vitabu hadi ramani, barua pepe hadi kupiga gumzo , Google imeshika karibu kila eneo la maisha ya kisasa. Kutoka ilivyoanzishwa ilikuwa ni mradi wa utafiti wa chuo kikuu, Google imejitokeza kuwa mradi mkubwa wa mabilioni ya dola ambao unakusanya kiasi kikubwa cha taarifa na takwimu kuhusu mamilioni ya watumiaji. Lakini taarifa zako za binafsi ni salama zikiwa katika mikono ya jabali hili la internet duniani? Anauliza mwandishi wetu Sarah Harman na taarifa yake inasomwa studioni na Sekione Kitojo.

Ilianza mwaka 1996 kama mradi wa shule wa wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Stanford.Miaka 13 baadaye , limekuwa shirika kubwa lenye thamani ya mabilioni ya dola, likiwa na wafanyakazi 20,000 duniani kote. Google ni chanzo cha utafutaji habari maarufu sana katika internet duniani , ikishughulikia zaidi ya asilimia 60 ya maulizo ya utafutaji habari na kadhalika.

Mafanikio ya kwanza ya Google ni kutokana na uwezo wa kusaka taarifa katika mtandao, ambayo ina kasi na sahihi zaidi kutoka washindani wake. Prof Neil Richards , profesa wa sheria katika chuo kikuu cha mjini Washington katika eneo la St. Lous , anakumbukia siku za mwanzo za Google.

Wakati ilipoanza ilikuwa tu chanzo cha kutafutia habari. Ina jina zuri na wavuti inayovutia. Hali hiyo ilionekana kufanyakazi, ilionekana kuwaongoza watu kupata habari wanazozitaka vizuri zaidi kuliko washindani wake.

Google hivi sasa inashughulikia zaidi ya maulizo milioni 200 kwa siku, ama tuseme kama theluthi mbili za maualizo yote katika internet. Msemaji wa Google Stephen Keuchel anajaribu kueleza kiwango cha wingi wa taarifa zinazoweza kupatikana katika Google.

Kila saa nne tuna orodhesha na kuongeza ama kupitia upya kiasi kikubwa cha takwimu kama kiwango chote cha taarifa katika maktaba ya baraza la Congress nchini Marekani, na hii ni kila baada ya saa nne.

Lakini licha ya kuwa neno hili Google limekuwa jina la upekuaji taarifa katika internet, hii leo kampuni hii inatoa huduma nyingine nyingi. Ukiwa umechoka kufuta barua pepe zako kadha katika kisanduku chako, basi jiandikishe na huduma ya google mail , Gmail, ambayo inawapa watumiaji kiwango kikubwa cha hifadhi ya barua zako pepe na vitu vingine. Kuna matumizi mengi ya katika google, baadhi yake tu ni kama You-Tube ambapo watumiaji wanaweza kutazama video mbali mbali.

Kama wavuti nyingi nyingine, google inaacha kitambuzi, ama cookies katika kompyuta ya mtumiaji, lakini tofauti na tuseme wavuti kwa ajili ya kununua vitu, google inaweza kufuatilia kila kina, mahali, na mada ambayo mtumiaji anaisaka. Kampuni inaweza kijifunza zaidi juu ya watu wanaotumia huduma zao, kama huduma ya barua pepe, Gmail ama wavuti ya masuala mtandao wa kijamii. Hivi karibuni kabisa , google imeshambuliwa na nchi kama Ujerumani na China kwa ajili ya mradi wake wa vitabu, ambao una lengo la kuweka mtandaoni mamilioni ya vitabu na kuweza kuvifanya kusomwa na kila mtu anayeweza kutembelea mtandaoni.

Mradi huo unaofanyika kuanzia nchini Marekani ni halali kabisa, anaeleza msemaji wa google Stephen Keuchel.

Kuna sheria nyingi za haki miliki nchini Ujerumani ikilinganishwa na Marekani. Tunaweza kuhamisha vitabu kutoka maktaba ambazo huenda bado zinakingwa na sheria hizi za haki miliki lakini kuna kitu katika sheria hizo nchini Marekani zinazoitwa matumizi ya haki na kifungu cha matumizi ya haki nchini Marekani kinaelezea hali ambayo mtu anaweza kunakili kitabu bila kwenda kinyume na haki miliki.

Wakati huo huo umoja wa Ulaya unapambana na google dhidi ya mpango wake huo wa kunakili vitabu kwa digitali. Umoja wa Ulaya unahofu kuwa iwapo utapata changamoto, mradi huo unaweza kuwa na maana kuwa kazi nyingi za watu wa Ulaya zitapatikana nchini Marekani.

Mwanmdishi Harman, Sarah / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri Mohammed Abdul Rahman