1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuendelea kwa mapigano kwakwamisha utoaji misaada, mashariki ya Congo.

Nyanza, Halima9 Novemba 2008

Juhudi zinaziofanywa na mashirika ya misaada kusaidia maelfu ya watu, zinakwama kutokana na mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, licha ya viongozi wa Afrika, kutaka kusitishwa mapigano.

https://p.dw.com/p/Fq43
kuendelea kwa vita Mashariki mwa Congo, kunazuia raia wasipate misaada ya chakula na madawa.Picha: AP

Afisa wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, Marcus Prior amesema wanahitaji haraka kwenda katika maeneo hayo yenye mapigano, kwa ajili ya kutoa msaada kwa raia.

Mapigano hayo kati ya Kundi la waasi linaloongozwa na Jenerali muasi Laurent Nkunda na wanamgambo wa Mai mai wanaodaiwa kusaidiwa na majeshi ya serikali, yameacha zaidi ya watu milioni moja bila ya makazi, katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na inakadiriwa kuwa watu laki mbili na hamsini wamepoteza makazi yao katika kipindi cha mwezi Septemba pekee, mwaka huu.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, imekuwa ikiilaumu Rwanda kusaidia kundi hilo la waasi linaloongozwa na Laurent Nkunda.

Hata hivyo Rwanda inapinga tuhuma hizo.

Waziri wa Habari wa Rwanda Louise Mushikiwabo wamesema wote wanaodai kuwa Rwanda inajihusisha moja kwa moja na kumuunga mkono Laurent Nkunda na kundi lake la CNDP, wanakosea.

Ameongeza kusema kuwa hiyo ni sababu moja wapo, kwanini mzozo huo haumaliziki kwa kutokana na sababu zinazobainishwa kuhusu mzozo huo kuwa si sahihi na kuongezab kuwa Laurent Nkunda ni raia wa Congo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na viongozi wa nchi za Maziwa Makuu, walikutana mjini Nairobi, siku ya Ijumaa katika juhudi zinazochukuliwa kidiplomasia, kumaliza mzozo huo.

Katika mkutano huo, viongozi wa Afrika wamelilaumu Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda amani kwa kushindwa kuwalinda raia wasio na hatia, ambapo raia wengi wanauawa kutokana na mapigano hayo.