1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kufuzu kwa Mkutano wa Mashariki ya Kati ni muhimu

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQG9

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amesema iwapo mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati wiki ijayo utafuzu utasaidia mazungumzo ya Israel na Wapalestina kufikia ufumbuzi kwa kuwepo kwa mataifa mawili.

Hata hivyo amesema majukumu yote yalioko kwenye rasimu ya mpango wa amani ulioandaliwa na Marekani,Urusi,Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya inabidi yatimizwe kwanza kabla ya kuundwa kwa taifa huru la Palestina.

Awamu ya kwanza ya mpango huo ambao ulikwama mara tu baada ya Bush kuuzinduwa hapo mwaka 2003 unajumuisha kusitishwa kwa vitendo vya ugaidi na umwagaji damu pamoja na harakati za Israel za kujenga makaazi ya walowezi wake.

Serikali ya Marekani imezialika nchi na mashirika 40 kuhudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika Jumanne ijayo huko Annapolis nchini Marekani.