Kugeuza kijivu hadi kijani: Kilimo cha mijini ulimwenguni
Kadri ambavyo miji imekuwepo, ndivyo ambavyo kilimo cha mjini kimekuwepo na kinaendelea kunawiri. Kutoka Berlin hadi Bangkok, wakaazi wanapanda vyakula kwenye paa na kubadili sura ya miji kutoka kijivu hadi kijani.
Uzinduzi wa kilimo cha mijini
Kwenye mabaraza, kuta, na hata makontena au sehemu zozote za wazi mjini, vinaweza kugeuzwa kuwa mashamba madogo. Ifikapo mwaka 2050, dunia itakuwa na takriban watu bilioni 10. Wawili kati ya watu watatu watakuwa wakiishi mjini. Changamoto kuu ya karne ya 21 inayokumbwa na mabadiliko ya tabia nchi na kuangamia kwa vitegemezi, ni kuwapa watu lishe bora. Hapo ndipo kilimo cha mjini kinaweza kusaidia.
Vidole vya kijani mijini
Wakaazi wa mjini wapendao mazingira asilia, wanazidi kukumbatia vijishamba vya mijini. Sababu za mwamko huu ni tele. Moja ni kuboresha maisha na kuimarisha muhusiano katika jamii. Nyingine ni kwamba kilimo cha mjini kinainua uchumi kwa kubuni nafasi za ajira na kuimarisha maendeleo ya bidhaa za kuuzwa hivyo kuhakikisha upatikanaji wa chakula.
Kupunguza joto mijini kutumia mimea
Kilimo cha mijini husaidia katika kupunguza viwango vya joto duniani na pia huongeza idadi ya viumbe hai katika miji yetu. Shamba la HK la Hong Kong lililoanzishwa Machi 2012 linajumuisha vijishamba kadhaa juu ya paa za nyumba eneo la Yau Ma Tei katika mtaa wa zamani wa Hong Kong. Kwa takriban nusu karne, eneo hilo halijashuhudia kilimo jinsi ilivyo sasa.
Kilimo juu angani
Shirika la Brooklyn Grange huongoza duniani katika kilimo cha kutumia udongo juu ya maghorofa mawili mjini New York. Kila mwaka wanapanda mimea asilia yenye uzito wa zaidi ya kilo 22,000. Pia wanayo zaidi ya mizinga 30 ya kuvuna asali juu ya paa za nyumba mjini humo. Walianza kilimo hiki mwaka 2010 kwa lengo la kutoa mfano endelevu wa kilimo cha mjini, kukuza mboga kwa jamii na kufaidi mazingira.
Kugeuza maeneo-taka kuwa mashamba
Prinzessinnengärten ulianzishwa kama mradi wa majaribio mwaka 2009 katika mtaa wa Kreuzberg mjini Berlin. Uliwekwa katika eneo lililotumika kutupa taka kwa nusu karne. Takataka zilitolewa kisha vipande vya mashamba vikaundwa. Kwa sasa ni mahali ambako watu wanagundua mengi kuhusu ulinzi wa tabia nchi. Wakati mwingine wadau hugeuza maeneo yaliyo wazi kama ya kujengea kuwa mashamba ya mjini.
Mpunga juu ya paa
Katika bustani moja iliyoko juu ya paa kwenye vijilima vya Roppongi ambayo pia ni eneo lenye maduka makubwa ya kibiashara mjini Tokyo- Japan, watu wamepanda mpunga kwenye mashamba ya pedi. Kwingineko katika mji huo, watu pia wanakuza tikitimaji, nyanya, soya na mchele kwa kutumia njia za asili ya majini lakini katika kilimo cha mjini.
Kuilisha jamii
Bustani ya kijamii ya Elliniko iliyoko nje ya mji wa Athens, ni kati ya ''bustani za kijeshi'' ambazo zimeshamiri Ugiriki wakati watu wakilemewa kupata chakula kufuatia hali ngumu za kiuchumi. Ipo katika uwanja wa zamani wa ndege ambao uliacha kutumika mwaka 2001. Watu waliojitolea walipanda matunda na mboga ili kusaidia wakaazi wa Athens wanaoongezeka na hutafuta chakula kwa familia zao.