1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuhamia teknolojia ya digitali Kenya bado changamoto

14 Januari 2014

Raia wa Kenya bado wana hofu na mchanganyiko wa kuhama kutoka matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia na kuhamia teknolojia ya digitali.

https://p.dw.com/p/1AqWx
Kuingia teknolojia ya digitali Kenya ni kitendawili.
Kuingia teknolojia ya digitali Kenya ni kitendawili.Picha: Fraunhofer ISE

Ifikapo mwaka 2015, muda ambao umepangwa na Umoja wa Mawasiliano ya Kimataifa Duniani kutawsitisha utangazaji wa kutumia analojia. Kuhamia teknolojia ya digitali kunalenga kuwapa huduma bora watumiaji, ingawa kwa nchi za Afrika Mashariki zoezi hilo limekuwa gumu na hivyo serikali husika kulazimika kuahirisha mara kadhaa.

Huku kesi ya kupinga uamuzi wa serikali wa kuvikatalia leseni ya matumizi ya digitali vyombo vya habari nchini Kenya haijamalizika, kesi ambayo ilifunguliwa na wamiliki wa vyombo vikuu vya habari nchini humo bado kuna masuala yaliyoibuka juu ya kuhamia tekenolojia ya digitali, ikiwa ni pamoja na malalamiko juu ya wachina kuchukua fursa kubwa ya kutawala vyombo vya habari, hasa kuelekea teknolojia ya digitali.

Lakini kwa Javas Bigambo, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Kenya, aliyebobea katika masuala ya vyombo vya habari , utawala na sera ameliambia shirika la habari la IPS kuwa halikuwa suala la bahati mbaya kwa serikali kuipa leseni ya digitali kampuni ya Kichina na kuwanyima wazawa, huku miundo mbinu ya kuanza kutumia digitali ikiwa bado haijatengenezwa.

Anasema mchambuzi huyo na hapa namnukuu "ikiwa bado tuna majonzi ya uamuzi wa Bunge kupitisha muswada tata kuhusu vyombo vya habari nchini humo wenye lengo la kudhibiti tasnia ya uandishi habari nchini bado serikali inaendelea kuyumbisha uhuru wa vyombo vya habari kwa hali ya juu", mwisho wa kumnukuu.

Walalamikia kampuni ya Kichina kupewa leseni

Kwa leseni hiyo, kampuni ya Kichina inayomilikiwa na mtandao wa Pan-Afrika –PANG na SIGNET-shirika la kimataifa la utangazaji , watakuwa na jukumu la kuwaunganisha watumiaji wa televisheni na televisheni hizo , ambapo pande zote zitahusika katika kurusha matangazo kwa makubaliano maalum na wamiliki wa vyombo vya habari, ambapo televisheni za ndani zitawajibika katika kutayarisha matangazo pekee.

Kwa upande wake Alex Gakuru ambaye ni mwenyekiti wa chama cha watumiaji wa mawasiliano ya teknolojia nchini Kenya na mjumbe wa kamati ya kusimamia uhamiaji kutoka analojia kwenda digitali amesema kumekuwa na hali ya wasi wasi kuwa kampuni hiyo ya kichina itadhibiti vyombo vya ndani vya habari na hivyo kudharau katiba na sheria za nchi, ingawa anasema hofu hizo zinapata ushawishi mbaya.

Amesema mawasiliano kwa umma ni suala la kisheria kwa mamlaka za mawasiliano na vyombo vya habari na kwamba kampuni hiyo ya kichina itakuwa na mamlaka ya kusambaza ving'amuzi vyenye kuonyesha chaneli zote cha televisheni za ndani na si kupendelea chaneli fulani,ikiwa itafanya hivyo itajiweka katika hatari ya kufungiwa leseni yake.

Grace Githaiga mdau wa mtandao wa mawasiliano ya teknolojia Kenya anasema kuwa ingawa kamisheni ya mawasiliano Kenya na mamlaka inayosimamia mawasiliao wamedai kuwa vyombo vya habari vya ndani hawakupata zabuni ya leseni ya digitali, hata hivyo vyombo hivyo vina kila sababu ya kulalamikia usimamizi wa kampuni ya kigeni wa digitali kwa kuwa wanaona wamevunjiwa haki yao.

Hata hivyo amasema wasi wasi juu ya kampuni hiyo ya Kichina kupewa leseni limetiwa chumvi kutokana na ukweli kwamba makamupni ya simu yanatumia tekenolojia ya kichina huku mamilioni ya watu wakiendelea kutumia vifaa vya umeme vinavyotengezwa au kununuliwa kutoka China.

Kampuni ya Kichina yalalamikiwa kupewa leseni.
Kampuni ya Kichina yalalamikiwa kupewa leseni.Picha: picture-alliance/dpa

Takwimu zilizotolewa na serikali zinaonyesha kuwa, shirika la habari la utangazaji la China, Xinhua husambazwa habari kwa watu milioni 17 wanaotumia simu nchini Kenya.

Lengo la teknolojia ya Digitali inayoendelea kuhimizwa kutumiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ni kutaka kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano kote duniani.

Teknolojia ya digitali kuongeza ubora

Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo, ongezeko la chaneli za televisheni litakalotokana na matumizi bora ya masafa, kuwepo kwa masafa ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwa mitambo ya analojia inayotumia masafa mengi.

Faida nyingine zilizobainishwa ni kuongezeka kwa watoa huduma wa mawasiliamo ya simu, matangazo ya televisheni kupatikana kwa vifaa vingi zaidi vya mawasilino kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa internet.

Mwandishi: Flora Nzema/IPS

Mhariri: Mohamed Khelef