1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuhamishiwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi wa Kenya huko Guantanamo

28 Machi 2007

Tume ya Haki za binaadamu ya Kenya imelaani vikali kuhamishiwa Guantanamo kwa mtuhumiwa wa ugaidi kutoka Kenya.

https://p.dw.com/p/CHHN
Shambulio la hoteli ya Mombasa
Shambulio la hoteli ya MombasaPicha: AP

Abdul Malik anatajwa kuhusika na shambulio la hoteli ya Mombasa lililouwa zaidi ya watu 12 hapo mwaka 2002 na jaribio la kudungua ndege ya Israel iliokuwa na abiria 271 karibu na Mombasa.

Mohamed Dahman alipata nafasi ya kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji ya tume hiyo Mwambi Mwaru ambaye anaielezea hatua hiyo ya serikali kuwa tata sio halali, inavunja haki za binaadmau, sheria za Kenya na za kimataifa.