1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya Ashura yaanza leo huko Karbala nchini Irak

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuGo

Waislamu wa madhehebu ya Shia leo wamekusanyika katika barabaa za mjini Karbala nchini Irak wengi wakijipiga migongo yao kutumia cheni za chuma huku sherehe ya Ashura ikianza kufikia kilele chake.

Usalama katika mji mtakatifu wa Karbala umeimarishwa huku mahujaji wakiruhusiwa kuingia mjini humo kupitia vituo maalumu.

Sherehe ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya mauji ya imamu Hussein na majeshi ya khalifa Yazid wa madhehebu ya Sunni mnamo mwaka wa 680, itafikia kilele chake hapo kesho Jumamosi.