1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuna mauaji ya kutisha CAR - Umoja wa Mataifa

Sekione Kitojo
31 Mei 2017

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonesha kutokea kwa uhalifu wa kutisha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ukiwemo ubakaji, mauaji, mateso, utekaji nyara na matumizi ya wanajeshi watoto, hali inayoweza kuwa uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/2dvXF
Zentralafrikanische Republik UN-Sicherheitstruppen in Bangui
Picha: picture-alliance/AA/Stringer

Umoja wa Mataifa umesema uhalifu wa kutisha katika muda wa miaka 12 kati ya mwaka 2003 na 2015 umefanywa na jeshi, makundi yenye silaha na majeshi ya kimataifa.

Ripoti hiyo, ambayo inaorodhesha pia visa vya bakaji, utumwa wa kingono, kuchoma moto kijiji kizima na hata mauaji ya kimbari yanayoweza kulingana na ya kimbari, ilitayarishwa kwa ajili ya mahakama mpya ambayo itaanzishwa mjini Bangui kuhukumu wahalifu. 

Katika ripoti nyengine ya Umoja wa Mataifa, inaarifiwa kuwa ghasia zinazoongezeka nchini humo zimesababisha vifo vya mamia ya watu pamoja na kuwalazimisha raia 88,000 kuyakimbia makaazi yao tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Idadi hiyo inawafanya watu waliokimbia makaazi yao ndani ya nchi hiyo kufikia watu 500,000.