1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la G-8

1 Juni 2007

kundi la G-8 la nchi tajiri ulimwenguni likijiandaa kwa mkutano wake huko Heiligendam,Ujerumani wiki ijayo linakumbana na vilio kujirekebisha na kuzijumuisha katika kundi hilo dola nyengine kuu zilizochomoza kama vile-China,India,Brazil na Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/CHkk

Kundi la G-8 la nchi tajiri za kiviwanda ulimwenguni sio klabu ya kila mtu.Mualiko wa kuhudhuria mikutano yake hutolewa kwa viongozi mashuhuri na wenye sauti duniani ama wakiume au wakike.

Viongozi wa dola na serikali wan chi hizo 8 watoka Ujerumani,Uingereza,Ufaransa,Marekani,Kanada,Japan,Itali na Russia.

Mkutano huu uliokua wa zamani sio rasmi na wa viongozi wa dola zenye nguvu kiuchumi duniani, umegeuka sasa taasisi rasmi.Lakini, huzijumuishi dola mpya zinazonyanyukia kiuchumi kama vile China na India na ajenda yao hupangwa na dola hizo 8.Swali ni je,desturi hii sasa sio imeshapitwa na wakati ?

Utandawazi-globalization-hauna maana kuwa na masoko huru isio na mipaka ulimwenguni bali pia kukabiliana na matatizo ya dunia na kuyapatia ufumbuzi kisiasa. Kushughulikia matatizo kama vile ya badiliko la hali ya hewa,ukosefu wa maendeleo,umasikini ulioenea duniani na kugawa raslimali ziliopo.

Kundi la G-8 kama dola kuu zenye nguvu kiuchumi ndio zina ushawishi mwingi ,lakini haziwezi kujiamulia mambo ya dunia hii peke yao.Hayo ni maoni ya dr.Sachin Chatuvedi-anaefanyia kazi taasisi ya kutunga fikra ,taftishi na habari kwa nchi changa mjini New Delhi, India:

Utandawazi tuliopitia sote katika nchi changa ni ule wa kibiashara.Taasisi hazikujiandaa kwa utandawazi wa aina hiyo na nikisema taasisi na kusudia umangimeza-nakusudia polisi,nakusudia mahkama,utaratibu wa kutunga sera katika nchi hizo haukujiandaa.Utandawazi uliangaliwa kwa jicho la kiuchumi tu .Kwahivyo, nchi hizi changa zinapaswa kwanza kudurusu kwa njia ya kuandaa taasisi zao kukabiliana bora zaidi na changamoto za utandawazi.”

Asema Chaturvedi .Hata ikiwa kundi hili la G-8 katika mkutano wao ujao huko Heiligendamm likizungumzia mada kama badiliko la hali ya hewa na misaada ya maendeleo,sauti hazitaacha kuzidi kupazwa ambazo zitaikatalia klabu hii ya “mabwana-wakubwa” uhalali wa kujiamulia wao tu na kupendekeza pekee ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili dunia hii.

Taasisi hii ya kundi la G-8 imepitwa na wakati adai Bibi Fatima Vianna Mello,mkurugenzi wa mpango wa kimataifa wa FASE-Jumuiya isio ya kiserikali ya hasama za kisiasa mjini rio de Jeneiro,Brazil:

Kwahivyo, tunapaswa kubadili mfumo wa maswali ya kimkakati na ya usalama ili tuwe na utawala wa demokrasia ya kweli duniani ili kukabiliana na hali hii ya hatari ya tunayoishi ulimwenguni.”

Asema Bibi Fatima Vianna Mello mjini Rio.

Hayo basi ndio maswali ambayo kundi la G-8 bila kujali limevinjari namna gani haliwezi kuyajibu.Mbali na hayo,ahadi lilizotoa katika mikutano yake iliopita hazikutekelezwa.

Hata ushawishi wa dola kuu zinazoinukia –kama vile China,India,Brazil,Mexico na Afrika Kusini, unapaswa kuzingatiwa na sio kusikilizwa pembezoni mwa mkutano tu.