1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la Hamas lapinga makubaliano ya mkutano wa Annapolis

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz8

Maelfu ya wafuasi wa kundi la Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza wamefanya maandamano makubwa katika barabara za mjini Gaza kuyapinga matokeo ya mkutano wa Annapolis nchini Marekani.

Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniya, amesema makubaliano yoyote yatakayofanywa na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas, hayatakubalika.

Haniya, ambaye alitimuliwa na rais Abbas kutoka kwa wadhifa wake wa uwaziri mkuu, amekataa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Wapalestina na Israel.

Muandamanaji mmoja ameuwawa mjini Hebron huko Ukingo wa magharibi wa mto Jordan wakati machafuko yalipozuka kati ya maafisa wa usalama walio watiifu kwa rais Mamhoud Abbas na wanamgambo wanaomuita msaliti.