1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la Hamas lapinga vikali nchi za kiarabu kushiriki mkutano wa Annapolis

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSkz

Kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza leo limelaani vikali uamuzi wa nchi kadhaa za kiarabu kuhudhuria mkutano kuhusu amani ya Mashariki ya Kati utakaofanyika tarehe 27 mwezi huu mjini Annapolis katika jimbo la Maryland, nchini Marekani.

Chama cha Hamas kimesema mkutano wa Annapolis utazipendelea sera za taifa la kiyahudi badala ya matakwa ya Wapalestina.

Kundi la Hamas ambalo haliitambui Israel, halikualikwa kwenye mkutano wa Annapolis. Kundi hilo lilijitengana na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, wakati lilipodhibiti eneo la Ukanda wa Gaza mwezi Juni mwaka huu.

Wakati huo huo, kundi hilo limetangaza katika tovuti yake kwenye mtandao wa internet kwamba litaongeza mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, mara tu mkutano wa mjini Annapolis utakapomalizika.