1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la mwisho la wanajeshi wa Marekani laondoka Iraq

18 Desemba 2011

Kundi la mwisho la wanajeshi wa Marekani waliyokuwepo nchini Iraq limeondoka asubuhi ya leo na kuvuka mpaka kuingia Kuweit, ikiwa karibu miaka tisa baada ya uvamizi uliomuondoa madarakani Saddam Hussein.

https://p.dw.com/p/13V2j
U.S. Army soldiers from the 1st Cavalry Division, the last soldiers to leave Iraq, arrive at Camp Virginia, Kuwait, Sunday, Dec. 18, 2011. The last U.S. soldiers rolled out of Iraq across the border into neighboring Kuwait at daybreak Sunday, whooping, fist bumping and hugging each other in a burst of joy and relief. (Foto:Gustavo Ferrari/AP/dapd)
Safari ya wanajeshi wa MarekaniPicha: dapd

Inakadiriwa magari 110 yaliwasafirisha askari hao, wengi wao wakiwa kutoka kikosi cha tatu na kundi la kwanza la askari wa farasi ambao walivuka mpaka majira ya saa 1:30 asubuhi. Hatua hiyo inafanya Iraq ibakiwe na askari kiasi cha mamia hivi katika ofisi za ubalozi wa Marekani. Iraq wakati mmoja iliwahi kuwa na karibu wanajeshi 170,000 wa Kimarekani katika kambi zipatazo 505. Kuondoka huko kunahitimisha mzozo na uvamizi wa kijeshi ambao ulianza kwa makombora kuushambulia mji wa Baghdad na kumalizikia kwa machafuko ya Iraq na mfumo wa demokrasia unaolegalega.

Mwandishi: Sudi Mnette