1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura juu ya kuiwekea vikwazo Iran yakhairishwa

1 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DG7m

LONDON

Uingereza na Ufaransa zimekhairisha shughuli ya kupiga kura katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya vikwazo dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa Kinuklia.Hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa nafasi zaidi kwa mataifa hayo kutafuta uungaji mkono zaidi wa azimio hilo.Ufarsansa na Uingereza zinahusika kufadhili azimio hilo ambalo litasababisha Iran kuwekewa duru ya tatu ya vikwazo baada ya taifa hilo kukataa kukomesha shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Libya,Indonesia,Afrika Kusini na Vietnam ambao sio wanachama wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa zinatilia shaka masuala kadhaa katika azimio hilo.Nchi nyingi za magharibi zinahofia kwamba Tehran inataka kutengeneza silaha za kinuklia lakini Iran iimesisitiza kwamba mpango wake sio kwa malengo mengine bali matumizi ya amani kwa ajili ya taifa lake.