1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni Sudan

25 Septemba 2010

Kura ya maoni nchini Sudan kufanyika Januari mwaka 2011.

https://p.dw.com/p/PMOl
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: AP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliungana na Rais Barack Obama kuitolea onyo Sudan kuhusiana na kura ya maoni itakayofanywa nchini humo. Katika Mkutano uliowaleta pamoja, jumuiya ya Afrika, Umoja wa Ulaya na viongozi wa mataifa ya Afrika, ikiwemo Sudan, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Obama alisema hatma ya mamilioni ya watu nchini Sudan inategemea namna kura hiyo ya maoni itakavyofanywa kwa uwazi, na kwa amani. Kura hiyo ya maoni ya Januari  mwakani, itawapa fursa wakaazi wa kusini mwa Sudan kupiga kura kuamua iwapo watatengana na serikali ya Khartoum ili kuunda serikali yao huru. Baadhi ya wanadiplomasia wanasema kura hiyo ya maoni imecheleweshwa, huku baadhi ya wachunguzi wakihofia iwapo itachelewehswa zaidi itazua mzozo mpya katika eneo hilo.