1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUra ya maoni ya rais nchini Syria

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxk

DAMASKUS:

Wapiga kura wa Syria wanateremka vituoni kuamua kama rais Bashar el Assad aendelee na wadhifa wake kwa kipindi chengine cha miaka sabaa.Rais Bashar el Assad ni mgombea pekee katika kura hiyo ya maoni.Upande wa upinzani unasusia zoezi hilo.Bashar el Assad,mwenye umri wa miaka 41 alichaguliwa miaka sabaa iliyopita kwa asili mia 97 baada ya babaake,Hafedh el Assad kufariki dunia mwezi mmoja kabla ya hapo.