1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zaanza kuhesabiwa nchini DRC

29 Novemba 2011

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura nchini DRC, huku hali ya usalama ikitajwa kuwa shwari katika mji mkuu Kishansa ambako jana kuliibuka machafuko.

https://p.dw.com/p/13Iqu
Maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya DRC wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Maafisa wa Tume ya Uchaguzi ya DRC wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.Picha: picture-alliance/dpa

Shughuli za kuhesabu kura zimeanza pia mashariki ya nchi hiyo, ambako nako pia hali ya usalama ni ya kuridhisha, baada ya kuripotiwa visa kadhaa vya ukosefu wa usalama jana (28.11.2011) usiku.

Mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo anaeleza hali ilivyo mchana huu mjini Kinshasa.

Pia Saumu Mwasimba amezungumza na makamu kiongozi wa Mashirika ya Kiraia ya Kutetea Haki za Binadamu ya Kivu Kaskazini, Omar Kavota, kuhusiana na matukio ya uvunjwaji wa haki za binaadamu ndani ya siku mbili za upigaji na uhisabuji kura.

Ripoti: Saleh Mwanamilongo
Mahaojiano: Saumu Mwasimba/Omar Kavota
Mhariri: Othman Miraji