1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zaendelea kuhesabiwa Sierraleone kukiwa na hali ya wasiwasi

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRY

Shughuli ya kuhesabu kura katika duru ya pili ya uchaguzi war ais inaendelea nchini Sierra Leone baada ya wananchi kupiga kura hapo jana.

Uchaguzi huo umekabiliwa na madai ya kutokea udanganyifu na kuzusha hali ya wasiwasi katika taifa hilo la Afrika magharibi ambalo limetoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika uchaguzi huo makamu war ais Solomon Berewa mwenye umri wa miaka 69 anakabiliwa na upinzani mkali wa kiongozi wa Upinzani Ernerst Koroma mwenye umri wa miaka 53.

Awali wagombea wote wawili walilalamika kwamba maafisa wa vyama vyao walikuwa wakinyanyaswa na polisi lakini hakuna waangalizi huru waliothibitisha madai hayo.

Mivutano ya kisiasa iliibuka wiki mbili zilizopita baada ya matokeo ya duru ya mwanzo ya uchaguzi huo kuonyesha kwamba mgombea wa chama tawala Solomon Berewa alikuwa wa pili akiwa na asilimia 38.3 huku Koroma akiongoza kwa kuwa na asilimia 44.3

Matokea ya mwanzo ya duru ya pili ya uchaguzi huu war ais yanatarajiwa kutangazwa kesho jumatatu.