1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zaendelea kuhesabiwa

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChZ9

NAIROBI:

Maofisa wa Kenya wanaendelea kuhesabu kura kufuatia uchaguzi wa urais na ubunge wa alhamisi.

Matokeo ya mwanzo yasio rasmi yanaonyesha Rais Mwai Kibaki kuwa nyuma ya mpinzani wake Raila Odinga.

Watu wengi walijitokeza katika uchaguzi uliofanyika alhamisi.Uchaguzi huo umeshuhudiwa na wachunguzi zaidi ya elf 15 kutoka umoja wa Ulaya na kanda ya Afrika Mashariki.

Miongoni mwa wachunguzi hao ni balozi wa Ujeruamni nchini Kenya-Walter Lindner.

Matokeo baado yanamiminika mjini Nairobi kutoka mikoani na kuhesabiwa kwa kura hizo na pia kutoa matokeo yote kunaweza kukaendelea hadi jumamosi.Kituo kimoja cha Televisheni cha Kenya KTN kimetangaza leo kuwa Bw Odinga alikuwa na kura zaidi ya millioni moja na laki nane huku rais Kibaki akiwa na kura millioni moja na zaidi ya laki moja.Rais Kibaki amewahimiza wananchi wa Kenya kusubiri matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi. Yeye mkuu wa polisi Mojammed Hussein Ali ameonya dhidi ya ghasia baada ya matokeo yote kutangazwa.