1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutetea ubingwa ngumu Uingereza, Conte

Sekione Kitojo
2 Oktoba 2017

Antonio Conte wa Chelsea asema kutetea ubingwa italia ni rahisi kuliko Uingereza.

https://p.dw.com/p/2l7OW
Fußball Länderspiel Deutschland - Italien
Antonio Conte wa ChelseaPicha: Reuters/M. Rehle

Kocha  mkuu  wa  Chelsea  Antonio Conte  anaamini kwamba  kutetea  ubingwa  wa  ligi  ni  jambo  rahisi  nchini Italia  kuliko  Uingereza  katika  Premier  League  kutokana na  sera  za  uhamisho  wa  wachezaji katika  vilabu vikubwa. Conte ameshinda ubingwa  mara  tatu  katika Serie A  nchini  Italia  akiwa  na  FC Juventus  baada  ya mahasimu  wao AC Milan  kuwauza  washambuliaji Zlatan Ibrahimovic, Alexandre Pato na  mlinzi Thiago Silva.

UEFA EURO 2016 Achtelfinale Italien vs. Spanien Trainer Antonio Conte
Antonio Conte kocha mkuu wa ChelseaPicha: Getty Images/AFP/M. Medina

Napoli iliwaondoa  winga Ezequiel Lavezzi  katika  kipindi cha  nyuma. Baada  ya  Chelsea  kushinda  ubingwa  wa ligi  msimu  uliopita mahasimu  wao  wakubwa Tottenham Hotspurs , Manchester City, Manchester United , Liverpool na  Arsenal , wamewekeza  pakubwa  katika  vikosi  vyao. Conte  alisema  ni  vigumu  kutetea  ubingwa  katika  ligi hiyo. Ni  vigumu  kushinda  mataji  mawili  mfululizo  katika ligi  ya  Uingereza.

Chelsea ilikubali  kipigo  cha  bao 1-0  dhidi  ya Manchester City siku  ya  Jumamosi , ambapo Man City ilipora uongozi wa  ligi  hiyo  kutoka  kwa  Manchester United  licha  ya  kushinda  kwa  mabao 4-0 dhidi  ya Crystal  Palece  siku  ya  Jumamosi.

Premier League - Watford vs Liverpool Trainer Jürgen Klopp
Kocha wa Liverpool Juergen KloppPicha: Reuters/Action Images/A. Couldridge

Kocha wa  Liverpool Juergen Klopp nae  ametathmini kushindwa  kwa  hivi  karibuni  kwa  kikosi  chake  kushinda katika  mchezo  wa  Premier League  baada  ya  sare  ya kufadhaisha  ya  bao 1-1 dhidi  ya  Newcastle United  kwa kusena , "soka halina usawa."

Kocha  huyo  raia  wa  Ujerumani  alipata  taabu  kuukubali ukweli  kwamba  kikosi  chake  kiliondoka  na  pointi  moja tu  baada  ya  kumiliki  mpira  kwa  muda  mrefu  dhidi  ya kikosi  cha  Rafa Benitez  cha  Newcastle  katika  uwanja wa  St. James Park jana  Jumapili.

Wakati  huo  huo  kocha  wa  Manchester United Jose Mourinho  amesema wachezaji  kadhaa  wa  kikosi  cha kwanza  kuwa  majeruhi  ni  fursa  kwa  wachezaji  wengine kujionesha  katika  kikosi  hicho  na  kupata  uzoefu.

Fußball Real Madrid - Manchester United
Paul Pogba wa Manchester UnitedPicha: Picture-alliance/dpa/N. Potts/PA Wire

Paul Pogba  ni  mmoja  wa  wachezaji  hao  ambao watakaa  nje  ya  uwanja  kwa  muda  mrefu, na  klabu hiyo  itakuwa  na  michezo  mitano  bila  ya  kiungo  huyo mchezeshaji, ikiwa  ni  pamoja  na mchezo walioshinda kwa  mabao 4-0 dhidi  ya  timu  iliyoko  mkiani ya  Crystal Palace.

Guardiola

Kocha  wa  zamani  wa  Barcelona  Pep Guardiola ameeleza  kushangazwa  kwake  leo na  ghasia  ambazo zimechafua  kura  ya  maoni  ya  kudai  kuwa  huru  kwa jimbo  la  Catalonia , ambazo  amesema  ingesababisha klabu ya  Barcelona  kuahirisha  mchezo  wake  dhidi  ya Las Palmas.

Demonstration für Unabhängiges Katalonien Pep Guardiola
Pep Guardiola akishiriki katika maandamano ya jimbo la Catalonia Picha: picture alliance/AP/dpa/E. Morenatti

Barcelona  iliishinda  Las Palmas  kwa  mabao  3-0  katika uwanja  ambao  ulikuwa  tupu  wa  Nou Camp jana Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe / ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman