1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuuliwa kwa wanyama pori nchini Tanzania

4 Januari 2012

Shirika la Kimataifa linalofadhili miradi ya kuwalinda wanyama Pori la TRAFFIC limesema kwamba mwaka 2011 ulikuwa ni mwaka mbaya kabisa kwa wanyama pori, hasa tembo ambao wameuliwa kwa kiasi kikubwa.

https://p.dw.com/p/13dcq
"wenn die touristen wegbleiben...." KT: 280708 Kenia Tourismus" Foto: Helle M Jeppesen
Idadi ya Tembo imepungua kiasi kikubwa nchini TanzaniaPicha: DW/Jeppesen

Inakadiriwa zaidi ya Tembo 3000 waliuwawa na wawindaji haramu. Shirika hilo linasema uwindaji haramu umefikia kiwango cha kutisha katika nchi za Kongo, Kaskazini mwa Kenya na Kusini mwa Tanzania pamoja na Msumbiji. Nchini Tanzania idadi ya wanyama hao imepungua kwa kiasi asilimia 42 katika kipindi cha miaka 3 kwa mujibu wa uchunguzi uliotolewa hii leo. Utafiti uliofanywa katika mbuga za Selous na Mikumi unaonyesha hadi mwaka 2009 idadi ya Tembo ilifikia 43,552 kutoka 74,900 katika mwaka 2006. Kutokana na hali hiyo, Sudi Mnette amezungumza na Meneja wa mradi wa wanyama pori katika shirika la WWF nchini Tanzania, Richard Rugemarira, ambaye kwanza ana haya ya kusema.

Mwandishi:Saumu Yusuf

Mhariri : Othman Miraji