1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuwait City. Kinu cha kusafishia mafuta chalipuliwa.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCw5

Mlipuko umetokea katika kituo kidogo cha kusafishia mafuta nchini Kuwait na kusababisha kufungwa.

Msemaji wa kampuni ya taifa ya petroli amesema kuwa mlipuko huo ulitokea mchana katika bomba la mafuta katika eneo la Shuaiba, kusini kidogo ya mji wa Kuwait City.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Kinu hicho cha kusafishia mafuta kimefungwa, lakini moto bado haujadhibitiwa.

Maafisa wamesema kuwa sababu za mlipuko huo zinachunguzwa.