1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUWAIT :Ziara ya Kansela Merkel yamalizikia Kuwait

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUR

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akikamilisha ziara yake katika Mashariki ya Kati amewasili nchini Kuwait.Hapo kabla alipokuwa nchini Umoja wa Falme za Kiarabu,Kansela Merkel alisisitiza dhima ya Umoja wa Ulaya,kutafuta suluhisho la amani kuhusu mgogoro wa Israel na Wapalestina. Alisema,ni muhimu kuwa na mtazamo wa kishujaa wenye suluhisho la kuwa na mataifa mawili.Wakati huo huo Merkel amezilaumu Syria na Iran kuwa zinazuia juhudi za amani katika Mashariki ya Kati.