1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUWAIT:Nchi za Kiarabu zaunga mkono mkakati wa Bush

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa5

Mkakati mpya wa rais George W.Bush wa Marekani kuhusu Irak umeungwa mkono na nchi nane za Kiarabu.Miongoni mwa nchi hizo ni Jordan, Misri,Saudi Arabia na Kuwait.Mawaziri wa kigeni wa nchi hizo nane za Kiarabu walipokutana na waziri mwenzao wa Marekani Bibi Condoleezza Rice nchini Kuwait,walieleza pia wasi wasi wao kuwa machafuko ya nchini Irak yanaweza kuenea katika eneo zima la Kiarabu.Vile vile ni matumaini yao kuwa hatua ya kupeleka vikosi zaidi vya Kimarekani itasaidia kuleta utulivu nchini Irak. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi nane za Kiarabu na Marekani imetoa mwito wa kuheshimu uhuru wa Irak.Mara kwa mara Iran na Syria zimelaumiwa kuwa zinawaunga mkono waasi nchini Irak.Juma lililopita Bush alitangaza mpango wa kupeleka Irak zaidi ya wanajeshi 20,000 wengine wa Kimarekani.