1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuwasili kwa waangalizi wa uchaguzi mkuu nchini DRC

5 Oktoba 2011

Waangalizi wa uchaguzi mkuu katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kutoka umoja wa Ulaya wameanza kuwasili mjini Kinshasa kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/12lsS
Uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo watarajiwa kufanyika Novemba,28,2011

Kwa jumla waangalizi 1,200 wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kufika nchini DRC. Wakati huo huo tume ya taifa ya uchaguzi inatarajia kuvunja mkataba na kampuni moja ya Ujerumani kutokana na uzembe katika uchapishaji wa karatasi za kupigia kura, na tume ya uchaguzi imependekeza karatasi hizo zichapishwe na kampuni kutoka China.

Taarifa zaidi ya mwandishi wetu kutoka Kinshasa Saleh Mwanamilongo.

Mwandishi: Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Josephat Charo