1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikwete anaamini ni sahihi Magufuli kuikosoa serikali yake

Seif Upupu29 Septemba 2015

Mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, wengi wanahoji tabia ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, kuomba kura kwa kulaumu serikali iliyopo sasa madarakani.

https://p.dw.com/p/1GfDJ
Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete (kushoto), akimtambulisha mgombea wa chake, John Magufuli.
Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete (kushoto), akimtambulisha mgombea wa chake, John Magufuli.Picha: picture-alliance/AP Photo/K. Said

Viongozi wa kisiasa wa vyama mbalimbali wanaendelea na kampeini zao kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 25 Oktoba. Hadi sasa, wagombea wanaotajwa kuwa na mchuano mkali ni wale wa chama kilichoko madarakani (CCM) na wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambao ni muungano wa vyama vya upinzani - CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.

Hata hivyo, kwa muda mrefu sasa, mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, amekuwa akitumia staili ya kuikosoa serikali ya chama chake kwenye kampeni zake, badala ya kutetea rikodi ya serikali hiyo inayoongozwa na Rais Jakaya Kkwete anayemaliza muda wake.

Katika mahojiano haya na meneja kampeni wa Magufuli, Abdallah Bulembo, mwandishi wetu wa Bukoba, Seif Upupu, anamuuliza meneja huyo juu ya staili hii ya kutoa lawama kwa serikali, ambayo yeye Magufuli alikuwa waziri.

Bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini kusikiliza mahojiano hayo

Mwandishi: Seif Upupu
Mhariri Mohammed Abdul-Rahman