1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwa uchache watu 71 wameuawa mjini Kismayo Somalia

Admin.WagnerD4 Julai 2013

Watu 71 wameuawa na wengine 300 wamejeruhiwa mjini Kismayo Somalia katika mapambano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa makundi ya waasi yanayohasimiana. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya ulimwenguni, WHO

https://p.dw.com/p/192Lx
FILE - In this Wednesday, Dec. 14, 2011 file photo, Kenyan army soldiers sit on a currently unused fishing boat on the white sand shore of the seaside town of Bur Garbo, Somalia. Kenya's military said Friday, Sept. 28, 2012 that its troops attacked Kismayo, the last remaining port city held by al-Qaida-linked al-Shabab insurgents in Somalia, during an overnight attack involving a beach landing. (AP Photo/Ben Curtis, File)
SomaliaPicha: dapd

Mapigano hayo katika mji wa bandari Kusini mwa Somalia yamesabisha watu wengi kuyahama makaazi yao na kuendelea kusababisha athari kubwa kwa wananchi na kukwamisha juhudi za utoaji wa misaada ya kibinaadamu katika eneo hilo.

Wahanga wengi wa mapigano hayo wamepata majeraha ya kuvunjika mifupa, vichwa na vifua ambapo kwa mujibu wa WHO karibu majeruhi 40 walilazimika kufanyiwa upasuaji.

Mji wa Kismayo kwa sasa ni uwanja wa mapambano kati ya wanamgambo wanaohasimiana wakipigania udhibiti wa mji huo muhimu kimkakati.

Serikali ya kuu ya Somalia kwa sasa inavinyoshea kidole cha lawama vikosi vya serikali ya Kenya ambavyo vimeweka kambi katika mji wa Kismayo kwa kuwasaidia wanamgambo wa kundi moja dhidi ya wengine na kuutaka umoja wa Afrika kutuma kikosi katika mji huo ambacho hakitaegemea upande wowote.

Serikali ya Somalia imelalamika kwa umoja wa Afrika kuwa mwenendo wa vikosi vya Kenya katika mji wa Kismayo vinahujumu juhudi za kijeshi za kupambanana na wapiganaji wa kiislamu wa kundi la al-Shabab.

Mbali na hilo vikosi vya Kenya vinashutumiwa kwa kuwasaidia wapiganaji wa kundi la Raskamboni Brigade, ambao walilisaidia jeshi hilo kuwafukuza wapiganji wa Al-shabab nje ya mji wa Kismayo.

Kundi hilo linaloongozwa na Ahmed Madobe, kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika maeneo yanayouzunguka mji wa Kismayo lakini asiyeungwa mkono na serikali kuu ya mjini Mogadishu. Jeshi hilo la Madobe linapigana na kundi lililokuwa likiongozwa na mbabe wa zamani wa kivita, Barre Hirale.

Mapema wiki hii wizara ya mambo ya nje ya Somalia iliuandikia barua Umoja wa Afrika kulalamika juu ya wanajeshi wa Kenya kuwa wamevuruga mipango ya kuwa na kikosi cha pamoja mjini humo kinachoongozwa na kamanda wa Somalia. Barua hiyo ilisema hatua hiyo imesababisha kuwepo kwa makundi mbalimbali ya kiukoo na hivyo kuzorotesha amani na usalama katika eneo la Jubba.

Mji wa Kismayo ni muhimu sana kwa serikali ya Kenya ambayo inataka ukanda wa kirafiki karibu na mpaka wake na Somalia, ikiwa ni moja ya sababu kuu za Kenya kutuma vikosi vyake kwenda Somalia kupambana na wanamgambo wa A-shabab mwaka 2011.

Lakini makundi ya waasi yanayopigana katika mji wa Kismayo yameoneka kuwa na hamu kubwa na injini ya mji huo wa Kismayo. Bandari ya mji hio huingiza pato kubwa la kutegemea na imetumiwa kusafirishia mkaa katika nchi za nje, bidhaa ambayo ilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa. 

Mwandishi: Hashim Gulana/ APE

Mhariri: Josephat Charo