1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KYOTO : Merkel ataka kupunguzwa kwa gesi chafu

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTs

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameyataka mataifa yanayoinukia kiuchumi kuweka malengo yalio wazi kuzuwiya kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Chini ya makubaliano ya Itifaki ya Kyoto ambayo muda wake unamalizika hapo mwaka 2012 nchi zinazoendelea kama vile China na India zilikuwa hazikulazimishwa kupunguza utowaji wa gesi hizo ambazo huchangia kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.

Kansela Merkel alikuwa akizungumza wakati akiwa ziarani mjini Kyoto ambapo ndipo mkataba wa Itifaki ya Kyoto ulitiwa saini.

Merkel anasema lazima wachukuwe juhudi za pamoja na nchi zinazoendelea wakati wa kulishughulikia suala hilo na kwamba hatimae nchi hizo zitimize ahadi zake kwani malengo ya kupunguza utowaji wa gesi hizo zenye kuathiri mazingira bado hayakufikiwa.

Japani ilikuwa ni kituo cha mwisho cha ziara ya Merkel barani Asia ambayo pia ilimfikisha nchini China.