1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS : Mripuko wa bomba la mafuta wauwa mamia

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfz

Mamia ya watu wameuwawa katika mripuko na moto kwenye bomba la mafuta lililotobolewa na wahuni katika mji mkubwa kabisa wa Nigeria Lagos hapo jana.

Moto huo ulizuka baada ya umma wa watu wa wakaazi wenyeji wa eneo lilipotokea tukio hilo wakiwahi kuchota mafuta kutoka kwenye bomba hilo ambalo lilitobolewa na wizi wanaoiba mafuta kwa kiwango kikubwa.Repoti juu ya idadi halisi ya maafa zinatafautiana sana lakini maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wanasema takriban watu 260 wameuwawa na wengine madarzeni kujeruhiwa.

Vuke kubwa la moto limewazuwiya wafanyakazi wa uokozi kuondowa maiti na inahofiwa kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka sana.

Vitendo vya kuiba mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta nchini Nigeria ni vya kawaida ambapo kuna uhaba wa mafuta licha ya kwamba nchi hiyo inashikilia nafasi ya nane kwa kusafirisha mafuta kwa wingi duniani.