1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagos: Wahanga wa mripuko wa bomba la mafuta wafanyiwa sala ya pamoja ya mazishi.

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfp

Mamia ya watu waliofariki kutokana na mripuko wa bomba la kupitishia mafuta wamefanyiwa sala ya pamoja ya mazishi mjini Lagos, Nigeria.

Waathiriwa hao waliangamia kwenye mripuko huo uliotokea wakati walipokuwa wakizoa mafuta ya petroli yaliyotoka kwenye bomba hilo lililokuwa limetobolewa na wezi wa mafuta.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu mia mbili na sitini na tisa waliuawa na wengine kadha wamejeruhiwa.

Hata hivyo, idadi hiyo bado ni ya kutiliwa shaka huku kukiwa na taarifa nyingine kwamba huenda waliofariki ni watu mia nane,

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, alielezea kusikitishwa kwake na habari za mkasa huo na akaahidi kwamba Umoja huo utajitahidi kusaidia kupunguza mikasa kama hiyo katika Afrika Magharibi.