1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS : Wanigeria wahofia uchaguzi wa ghasia

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9J

Wanigeria wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria wa rais hapo Jumamosi siku kadhaa baada ya chaguzi za majimbo kupelekea kuuwawa kwa zaidi ya watu 20 na Mahkama Kuu kumrudisha makamo wa rais Atiku Abubakar katika orodha ya wagombea.

Uchaguzi wa kurithi nafasi ya generali wa zamani Olesegun Obasanjo unapaswa kuwasilisha makabidhiano ya kwanza ya utawala mmoja wa kiraia kwenda kwa mwengine tokea taifa hilo kubwa barani Afrika lijipatie uhuru wake hapo mwaka 1960.

Lakini wasi wasi wa kiafya kwa mrithi alieteuliwa kushika nafasi ya Obasanjo Umaru Yar’Adua na mzozo juu ya madai ya rushwa dhidi ya makamo wa rais Atiku Abubakar yameweyakea kiwingu matokeo ya uchaguzi huo.

Jimbo kubwa kabisa la Nigeria la Kano pamoja na majimbo ya Ondo na Bauchi yamewekwa chini ya amri ya kutotembea baada ya uchaguzi wa magavana Jumamosi iliopita kuchchea umwagaji damu na kuuwawa takriban watu 21.