1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lahti, Finnland. Viongozi wa Ulaya kujadili nishati na usalama.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0s

Viongozi wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana katika mji wa Lahti nchini Finland baadaye leo kwa mazungumzo yanayotarajiwa kulenga katika suala la kuzidi kwa ujoto duniani, uchafuzi wa hali ya hewa pamoja na usalama.

Finland ambayo hivi sasa inashikilia urais wa umoja wa Ulaya, imemwalika rais wa Russia , Vladimir Putin kujadili ushirikiano wa muda mrefu kuhusu nishati na viongozi wa kundi hilo la mataifa 25 wanachama wa umoja wa Ulaya.

Lakini viongozi hao wa umoja wa Ulaya pia wanatarajiwa kuzusha suala la demokrasia nchini Russia pamoja na hatua za Russia dhidi ya Georgia pamoja na kifo cha hivi karibuni cha mwandishi habari za kiuchunguzi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Russia.