1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAHTI: Putin akataa kusaini mkataba na Umoja wa Ulaya

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0V

Rais wa Urusi Vladamir amekataa takwa la kusaiani mkataba wa nishati wa kimatafia na Umoja wa Ulaya, akisema sekta zote haziwezi kuzungumziwa katika mkataba mmoja.

Rais Putin ameyasema hayo kufuatia mkutano wake na viongozi wa nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya mjini Larti Helsinki jana jioni. Hata hivyo rais Putin amesema Urusi itaheshimu majukumu yake kwa mataifa ya Umoja wa Ulaya na kuhakikisha ugavi wa mafuta na gesi unaendelea bila kutatizwa.

Mataifa ya Umoja wa Uklaa yanaitaka Urusi iwe wazi zaidi kuhusiana na swala la nishati, huku nchi hiyo ikiwa mgawaji mkubwa wa mafuta na gesi barani Ulaya, ikitosheleza asilimia 25 ya mahitaji ya Ulaya.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema Umoja wa Ulaya na Urusi zitafaidi kwa kuyafungua masoko yao. Mzozo kati ya Urusi na Ukraine wakati wa kipindi cha baridi kilichopita, uliathiri ugavi wa gesi barani Ulaya.