1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Leipzig wakosolewa

Oumilkheir Hamidou
14 Oktoba 2016

Baada ya kisa cha kujinyonga jela gaidi mtuhumiwa wa Jaber al-Bakr mjini Leipzig,polisi na wanasiasa wanajikuta wakizidi kutiwa vishindo. Kansela Angela Merkel amehimiza uchunguzi kamili ufanywe kuhusu kisa hicho.

https://p.dw.com/p/2RFE3
Deutschland Terrorverdächtiger Al-Bakr erhängt in Zelle aufgefunden
Picha: picture-alliance/dpa/S. Willnow

"Yadhihirika kana kwamba katika jela hiyo kuna kilichokwenda kombo na tathmini ya hali ya mambo haikuwa sahihi",amesema hayo msemaji wa serikali Steffen Seibert."Muhimu ni kwamba uchunguzi wa kina unaendelea. "Nini kimefanyika vibaya,kipi kimekadiriwa sivyo?" Ingawa waziri mkuu wa jimbo la Saxony Stanislaw Tillich amekiri  makosa yametokea,hata hivyo anapinga yeye binafsi kubeba jukumu angalao kwa sasa la yaliyotokea. Kisa hicho kinabidi kwanza kichunguzwe amesema mwanasiasa huyo wa chama cha Christian Democratic CDU akiwa mjini Berlin.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka katika mji wa Leipzig,uchunguzi wa maiti ya  mtuhumiwa umebainisha amejiuwa.

"Mfungwa anapojiuwa daima ni jambo baya" amesema msemaji wa kansela Merkel. Katika kisa hiki shughuli za wachunguzi wa polisi kuhusu kifo cha kijana wa miaka 22 zitazidi kuwa ngumu. Hali hiyo inazusha masuala kuhusu nani walikuwa nyuma yake na pia kuhusu njia aliyopitia hadi kugeuka kuwa mfuasi wa itikadi kali."

Mkuu wa jela ya Leipzig Rolf Jacob anajieleza mbele ya waandishi habari
Mkuu wa jela ya Leipzig Rolf Jacob anajieleza mbele ya waandishi habariPicha: picture-alliance/dpa/A. Burgi

Lawama zimetolewa pia na waziri wa ndani de Maizière

"Kisa kimeshakabidhiwa vyombo vya sheria. Uchunguzi ungali bado unaendelea na nnaweza kukuhakikishieni kwamba wahusika wenyewe katika jimbo la Saxony wanaitambua kazi kubwa inawasubiri."Amesema hayo wa mambo ya ndani Thomas de Maizière.

Maafisa wa usalama sawa na maafisa wa serikali katika jimbo la Saxony wamekuwa kila mara wakilaumiwa. Wanatuhumiwa miongoni mwa mengineyo kufanya uzembe katika kukabiliana na makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia na kuvifumbia macho visa vinavyofanywa na wafuasi wa makundi hayo. Baada ya kujiuwa Al Bakr wanasiasa wa vyama vyote wanawalaumu maafisa wa serikali ya jimbo la Saxony.

Vijana wa Syria waliomkamata al Bakr wanahofia maisha yao

Jaber al-Bakr amefungwa miguu na mikono na wasyria wenzake kabla ya kukabidhiwa polisi
Jaber al-Bakr amefungwa miguu na mikono na wasyria wenzake kabla ya kukabidhiwa polisiPicha: Facebook/Syrische Gemeinde in Deutschland

Lawama zimesikika pia kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu ambayo imeamua kuishughulikia kadhia hiyo hivi sasa. Mtandao wa vyombo vya habari vya Ujerumani vimenukuu duru za usalama zikisema mtuhumiwa huyo wa kigaidi hakuhojiwa alipoingia katika jela ya Leipzig. Suala watu wanalojiuliza ni kwa nini kijana huyo amesalia muda mrefu  katika jela ya Leipzig badala ya kuhamishiwa Karlsruhe yanakokutikana makao makuu ya mwendesha mashitaka mkuu?

Mpaka vijana wa Syria waliomkamata mtuhumiwa huyo wanawalaumu maafisa wa serikali mjini Leipzig. Wanapokea vitisho watauliwa na wanamgambo wa dola la kiislam IS-mmojawao ameliambia gazeti la Bild. Hawana kinga anasema na kukanusha wakati huo huo tuhuma za Al Bakr eti walikuwa wakijua kuhusu mipango ya kufanywa mashambulio.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters

Mhariri: Gakuba Daniel